Serikali ya Marekani yaimarisha mifumo ya afya inayolenga kumaliza janga la VVU nchini Tanzania

Press Release Shim

Speeches Shim

Serikali ya Marekani yaimarisha mifumo ya afya inayolenga kumaliza janga la VVU nchini Tanzania
Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP)
Erick Gibson / JSI

For Immediate Release

Friday, 17 July, 2020

Dar es salaam: Julai 16, wawakilishi kutoka Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania walishiriki katika kikao-mtandao ambapo walijadili mafanikio na hatua za kuchukua siku zijazo ili kuimarisha  mifumo ya afya nchini Tanzania, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP).

Mradi wa USAID wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP) ulitumia njia ya kuimarisha mifumo sambamba na malengo ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi kusaidia Serikali ya Tanzania kudhibiti janga la VVU.

Mradi wa CHSSP wa miaka sita wenye thamani ya dola za Marekani milioni 36, umetoa mafunzo kwa watoa huduma wa kujitolea ngazi ya jamii zaidi ya elfu kumi na nane (18,000) na kujenga uwezo wa mashirika 49 ya asasi za kiraia. CHSSP pia iliboresha maelfu ya mifumo ya jamii ya serikali za mitaa kote nchini ili kuweza kubaini idadi ya watu walio hatarini, wafanyiwe vipimo, waunganishwe na huduma za matunzo, na kubakia katika matibabu.

Kutokana na matokeo ya jitihada hizi, mradi uliwafikia watu zaidi ya milioni 1 katika halmashauri 106 za Tanzania kwa upimaji wa VVU, ambapo asilimia tisini (90%) ya waliobainika kuwa na maambukizi walianzishiwa matibabu ya VVU. Zaidi ya watoto laki saba (700,000) na familia zinazoishi katika mazingira hatarishi sasa wameunganishwa na huduma za kuokoa maisha na ustawi wa jamii. Haya ni matokeo yanayoonekana ambayo yanachangia moja kwa moja kufikia malengo ya 90-90-90 ya kumaliza janga la VVU (asilimia 90 ya watu wote wanaoishi na VVU wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 ya watu wote waliogundulika na VVU wanapata huduma endelevu ya tiba ya kuongeza kinga ya mwili, na asilimia 90 ya watu walio kwenye tiba ya kuongeza kinga ya mwili wanakuwa na kiwango kidogo sana cha virusi vya UKIMWI, yaani virusi vinafubazwa.

Wakati wa mkutano wa kufunga mradi kupitia kikao-mtandao, Mkurugenzi Mkazi wa USAID wa Tanzania, Andrew Karas, alisema “Marekani ipo sambamba na watu wa Tanzania katika kujitolea kwao kuendelea kujenga mifumo ya afya ya jamii na kutokomeza maambukizi ya VVU. Kwa kuendeleza ushirikiano katika kuzuia, kutoa matunzo na matibabu, tutafikia lengo la kizazi kisichokuwa na UKIMWI. "

Ili kupata taarifa zaidi, tafadhali piga simu Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kupitia: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.