Press Release Shim
Speeches Shim
For Immediate Release
Dar es Salaam: Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 2.4 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5.6), ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya nchini Tanzania. Msaada huu unalenga kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara (laboratory capacity for optimal diagnostics), kusaidia jitihada za utoaji taarifa (risk communication) , miradi ya maji na usafi wa mazingira (water and sanitation), kuzuia na kudhibiti maambukizi, kutoa elimu ya afya kwa umma (public health messaging) na miradi mingine. Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4. Isitoshe, kiasi kingine cha Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimebadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya janga hili. Hii inafanya jumla ya fedha zote zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na COVID-19 nchini Tanzania hadi hivi sasa kufikia Dola za Kimarekani milioni 5.3 (Sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 12.2).
Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita Marekani imewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 7.5 kwa maendeleo ya Tanzania huku karibu Dola za Kimarekani bilioni 4.9 zikielekezwa kwenye sekta ya afya pekee. Toka mwaka 2009 Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 100 kusaidia miradi ya afya na takriban Dola za Kimarekani bilioni 70 kama msaada wa kibinadamu duniani kote. Serikali ya Marekani inaendelea kuwa mfadhili mkubwa zaidi duniani wa miradi ya afya na shughuli za kibinadamu zinazolenga maendeleo ya muda mrefu na jitihada za washirika wake kujijengea uwezo na kuchukua hatua za dharura wakati wa majanga. Aidha tunaongoza duniani katika utoaji wa misaada ya kibinadamu na kiafya katika kukabiliana na janga la COVID-19.
Marekani inaendelea kuonyesha uongozi katika jitihada za kimataifa za kukabiliana na janga la COVID-19. Watu wa Marekani wametoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 10 zitakazosaidia jitihada za kimataifa za kukabiliana na COVID-19. Aidha, tutaendelea kuhakikisha kuwa mchango mkubwa wa kifedha na wa kisayansi wa Marekani katika mapambano haya unabaki kuwa kitovu na sehemu ya jitihada za pamoja na zilizoratibiwa vyema za jumuiya ya kimataifa dhidi ya COVID-19. Ikiwa ni miezi kadhaa sasa tukipambana na janga hili nchini kwetu na nje ya nchi yetu, Marekani inaendelea kuongoza jitihada za kimataifa dhidi ya mlipuko huu, ikijenga katika uzoefu wa miongo kadhaa ya uongozi katika utoaji misaada ya kiafya inayookoa maisha na misaada ya kibinadamu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa Simu: +255 22 229-4000 au kwa barua-pepe: DPO@state.gov.
###
Comment
Make a general inquiry or suggest an improvement.