Taarifa ya Waache Wasome

Speeches Shim

Waache Wasome ni mradi wa miaka mitano ambao unakusudia kuongeza ushiriki na kuhakikisha wasichana walio katika rika balehe wanabakia shuleni katika shule za sekondari. Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuongeza viwango vya ushiriki wa wasichana kwa shule za sekondari. Walakini, wakati idadi kubwa ya wavulana na wasichana inaanza kidato cha kwanza kila mwaka, mwisho wa miaka minne, wasichana wengi hawatakuwa tena shuleni. Jitihada za Waache Wasome zimewekwa katika misingi ya kuwawezesha wasichana kuunda na kufikia malengo kwa mustakabali wa maisha yao, wakati wa kushughulikia masuala ya kijamii / jinsia, vizuizi vya kiuchumi, na ukatili vinavyozuia uwezo wao wa kubaki na kufanikiwa shuleni.

Date 
31-10-2018 08:30